- NEWS & PUBLICATIONS

Back

DENMARK YATOA VIFAA VYA KISASA KWA TRA KUSAJILI WALIPA KODI

Serikali ya Denmark kwa kushirikiana na mradi wa kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji (LIC),  wametoa mashine za kutengenezea vyeti vya walipa kodi, kwa vituo kumi na tatu(13) vilivyojengwa ndani ya halmashauri za mikoa ya Dodoma na Kigoma.

Vitakavyo tumika na Mamlaka ya  Mapato Tanzania, TRA, kutoa elimu kwa mlipa kodi, na vyenye thamani ya zaidi ya milioni mia moja sitini na saba(167), lengo  likiwa ni kuboresha mazingira ya biashara na udhibiti wa upotevu wa mapato.

Akipokea vifaa hivyo Jijini Dodoma, katibu mkuu, Wizara ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI, Joseph Nyamhanga, amesema msaada huo utasaidia katika juhudi za serikali katika mapambano na kudhibiti upotevu wa mapato.

Amesema vifaa hivyo itakuwa msaada mkubwa katika kuandaa takwimu zitakazopatikana ndani ya vituo vya uwekezaji vilivyojengwa katika halmashauri za mikoa ya Dodoma na Kigoma, ambazo pia zinazohusiana na biashara na uwekezaji, ikiwa ni pamoja na kujua bidhaa zinazozalishwa katika maeneo husika.

“Tumejenga vituo vya kutoa elimu kwa mlipa kodi, kwa msaada huu utasaidia tujue takwimu sahihi zitakazopatikana ndani ya vituo hivi tulivyovijenga ili kutoa elimu kwa mlipa kodi ambapo kwa kuanza tumejenga halmashauri za mikoa ya Dodoma na Kigoma na baadaye tunaenda katika mikoa mingine” amesema Nyamhanga.

Amesema vituo hivyo ambavyo vitatumika kutoa elimu kwa mlipa kodi, vitakuwa msaada mkubwa kwa wananchi waliokuwa wakitoka halmashauri moja kwenda makao makuu ya mikoa kupata huduma hiyo.

Donald Liya ambaye ni mshauri wa mazingira ya biashara na uwekezaji, amesema kabla ya ujenzi wa vituo hivyo walifanya utafiti na kugundua kuwa kwa halmashuri za Kigoma na Dodoma, asilimia 87% ya biashara hazijarasimishwa.

Hivyo serikali inapoteza mapato mengi, na wao wanakosa takwimu sahihi za biashara zilizopo katika eneo husika, hivyo wakaamua kujenga vituo hivyo ili biashara nyingi ziweze kurasimishwa.

Na kupitia vituo hivyo halmashauri husika ziweze kupata mapato husika na kurahisisha urasimishwaji wa biashara.

Vilevile ametaja vifaa vilivyonunuliwa pamoja na mashine hizo ni finger Print ya vidole vinne, na ya kidole gumba, kamera na kompyuta  mpakato, ambavyo vitakuwa vikizunguka vijiji vyote ndani ya halmashauri husika.

Nae kamishna wa TRA, Charles Kichele mbali na kuishukuru serikali ya Denmark, kwa kupatiwa vifaa hivyo ambavyo vitasaidia wao kuongeza walipa kodi zaidi, vilevile amesema wataendelea kushirikiana na TAMISEMI, ili kuwafikia walipa kodi wengi zaidi kwa sababu TAMISEMI wanafika hadi ngazi za mitaa ambapo wao hawajafika.

“Tunaishukuru serikali ya Denmark kwa msaada huu vifaa hivi vitatusaidia sana kuongeza walipa kodi zaidi na lengo letu ni kuwafikia walipa kodi wengi, na kwa kushirikiana na TAMISEMI naamini tutawafikia walipa kodi wengi zaidi kwa sababu wapo hadi ngazi za mitaa ambapo sisi hatujafika huko” amesema  Kichele.

Amesema watawafikia watu wengi zaidi kwa sababu upatikanaji wa leseni za biashara utakuwa rahisi sana na itapatikana ndani ya siku moja tu.

Pia amekanusha uvumi wa kuwa TRA wanachukua kodi hata kabla ya kufanya biashara, amesema wafanya biashara wamekuwa wakilipa kwa robo ya mwaka, au miezi sita, na wapo kwenye mchakato wa mfanyabiashara alipe mwisho wa mwaka baada ya kufanya biashara.

Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI Tixon Nzunda kuanzia kushoto, Kamishna wa TRA Charles Kichele, Katibu Mkuu TAMISEMI Joseph Nyamhanga, na Mshauri wa mazingira ya biashara na uwekezaji Donald Liya, wakiwa wameshika begi lenye vifaa wakati wa hafla ya makabidhiano.

Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI Tixon Nzunda kuanzia kushoto, Kamishna wa TRA Charles Kichele, Katibu Mkuu TAMISEMI Joseph Nyamhanga, na Mshauri wa mazingira ya biashara na uwekezaji Donald Liya, wakiwa wameshika begi lenye vifaa wakati wa hafla ya makabidhiano.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Makala na, EZEKIEL  NASHON, DODOMA. 

Link: jmabula blog